IRAN

Sherehe za kuapishwa raisi mpya wa Iran Hassan Rouhan kufanyika leo

Raisi Mpya wa Iran Hassan Rohan ambaye anachukua nafasi ya Ahmed Nejad,sherehe za kuapishwa kufanyika jumapiliی
Raisi Mpya wa Iran Hassan Rohan ambaye anachukua nafasi ya Ahmed Nejad,sherehe za kuapishwa kufanyika jumapiliی DR

Nchini Iran Hasan Rouhani amekabidhiwa rasmi kiti cha uraisi ambacho kilikaliwa na mahmod ahmed nejad kama raisi wa taifa hilo ambapo sasa ameahidi kushughulikia masuala ya uchumi wa taifa hilo sambamba na vikwazo dhidi ya taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Bwana Rowhani anakabidhiwa nafasi hiyo baada ya ushindi alioupata mwezi june alipoahidi kufanya mageuzi na kukomesha taifa hilo kutengwa kimataifa.

Sherehe za makabidhiano ya madaraka sambamba na shughuli hasa za kuapishwa zinafanyika leo jumapili ambapo takribani viongozi kumi kutoka mataifa mbalimbali watahudhuria.

Kiongozi huyo mwenye umri wa mika 64 alikuwa mjumbe wa zamani wa masuala ya nyuklia ya taifa hilo na mwanaharakati wa kiislamu kabla ya mapinduzi ya mwaka 1979.