SYRIA

Assad asema mgogoro wa Syria utamalizwa kwa kuondoa ugaidi

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad worldpress.com

Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema kuwa mgogoro wa Syria unaweza kutatuliwa kwa kufutilia mbali ugaidi, akimaanisaha waasi wanaopambana na serikali yake. 

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake nadra kwenye televisheni ya taifa hilo jana Jumapili, Assad aliukosoa upinzani wa kisiasa dhidi ya utawala wake na kuulezea kushindwa na kwamba hauna nafasi yoyote katika kutatua vita ya kikatili nchini humo

Assad ameongeza kuwa hakuna suluhu inayoweza kufikiwa pamoja na waasi isipokuwa kwa kupambana nao kwa ngumi ya chuma na kwamba hatua ya sasa si ya kutafuta suluhu bali kuwafutilia mbali.

Mnamo Machi 2011, maandamano makubwa yalienea maeneo mbalimbali kwa ajili ya wito wa mabadiliko ya kisiasa nchini Syria ambapo hadi hivi sasa maelfu ya raia wamepoteza maisha.