Zimbabwe

Mugabe kuapishwa Jumatano hii ikiwa MDC haitapeleka kesi mahakamani hii leo

Rais mteule wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais mteule wa Zimbabwe Robert Mugabe rfi

Rais mteule wa Zimbabwe Robert Mubage ataapishwa siku ya Jumatano ikiwa chama cha Movement for Democratic Change hakitawasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa Mugabe uliotanagzwa Jumapili iliyopita. 

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa MDC itawasilisha kesi Mahakamani ya kupinga matokeo hayo, Mugabe atasubiri siku saba kabla ya kuapishwa.

Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema hawezi kutambua ushindi wa rais Mugabe wa asilimia 61 kwa kile alichokisema kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Waangalizi wanasema licha ya uchaguzi huo kuwa huru, tume ya uchaguzi inastahili kufanyiwa marekebisho.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ZEC inatuhumiwa kuongeza mara mbili zaidi karatasi za kupigia kura na kufikia milioni 8.6 badala ya milioni 6.5 ya idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura