IRAN

Umoja wa Ulaya wamtaka rais mpya wa Iran kuharakisha utatuzi wa mgogoro wa mpango wa Nyuklia.

Rais wa Iran Hassan Rohani.
Rais wa Iran Hassan Rohani. AFP PHOTO/BEHROUZ MEHRI

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa rais mpya wa Iran Hassan Rowhan kupiga hatua za haraka kuelekea katika kutatua wasiwasi wa mpango wa nyuklia unaoleta mgogoro baina ya taifa hilo na mataifa mengine baada ya kupinga msimamo wa maridhiano. 

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Magaharibi yana matumaini kwamba rais Rowhani atachukua hatua za kujenga zaidi katika mazungumzo ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuhusu mpango wa nyuklia licha ya Irani kukanusha shutuma za mataifa yenye nguvu kuwa na malengo ya kijeshi.

Jana Jumapili, rais Rowhani alirudia kampeni yake ya ahadi ya kuwasaidia Wairani ambao wanataabika chini ya uzito wa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani na Umoja wa Ulaya EU na kutoa wito kwa ajili ya kuheshimiana na mataifa ya Magharibi,akionesha nia ya kupambana tofauti na mtangulizi wake.

Mataifa ya Magharibi yanaamini kuwa mpango wa nyuklia wa Iran unatumika kuendeleza bomu la atomiki, lakini Tehran inasisitiza ni kwa madhumuni ya amani.