ZIMBABWE

Chama cha MDC kupinga mahakamani matokeo ya urais nchini Zimbabwe kabla ya siku ya Ijumaa

Kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai
Kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai zimbanewsonline.com

Waziri mkuu wa Zimbabwe ambaye ameshindwa katika kinyang'anyiro cha uraisi Morgan Tsvangirai amejiandaa kupinga matokeo yaliyompa ushindi raisi Mugabe kwa kufuata taratibu za mahakamani.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Tsvangirai wamesema wataanza harakati rasmi kwa mujibu wa katiba kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jumatano, ambayo yalimpa Mugabe ushindi wa asilimia 61 ya kura zote.

Msemaji wa chama cha MDC Douglas Mwonzora amebainisha wanasheria wa chama cha MDC wanajituma kuhakikisha kabla ya Ijumaa harakati hizo kuwa mahakamani.

Madai ya upinzani yatazuia kuapishwa kwa raisi mugabe kukalia kiti hicho kwa awamu nyingine.

Endapo Mugabe ataapishwa kuwa rais hii itakuwa awamu yake ya saba katika uongozi wa taifa hilo ambapo amedumu madarakani kwa miaka 33 akiwa rais mkongwe zaidi kukaa madarakani barani Afrika.