MISRI

Maseneta wawili wa Marekani wawasili Misri kushiriki jitihada za kuleta amani nchini humo

Maseneta wa Marekani John McCain na Lindsey Graham
Maseneta wa Marekani John McCain na Lindsey Graham politico.com

Jitihada za kidiplomasia zinaendelea kufanyika ili kutanzua mgogoro wa kisiasa nchini Misri kwa naibu waziri wa mambo ya kigeni wa marekani William Burns kumtembelea naibu kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood Khairat al-Shater aliyeko gerezani. 

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kiongozi huyo wa Muslim Brotherhood alikatisha ziara ya naibu waziri Burns kwa kusema wanapaswa kukutana na raisi Morsi aliyeondolewa madarakani badala ya kumtembelea yeye.

Misri imerejea katika hali ya sintofahamu baada ya Jeshi kumuondoa madarakani raisi Mohamed Morsi na maelfu ya wafuasi wake kuandamana katika miji miwili wakidai kiongozi huyo wa Muslim Brotherhood arejeshwe mamlakani.

Kufuatia jitihada za kidiplomasia kuimarishwa ili kutatua mzozo nchini humo tayari maseneta wa marekani John McCain na Lindsey Graham wamewasili mjini Cairo jana Jumatatu kushiriki mazungumzo ya siku mbili.