MAREKANI

Mawasiliano ya viongozi wa Al Qaeda chanzo cha balozi za Marekani kufungwa

Kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri
Kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri coolimages786.blogspot.co.nz

Imebanika kuwa mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa Al Qeada akiwemo Ayman al-Zawahiri kiongozi wa kundi hilo yalisababisha Marekani kuamua kufunga balozi zake Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kuanzia siku ya Jumapili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa shirika la Ujasusi nchini humo lilifanikiwa kunasa mawasiliano hayo kabla ya hatua kuchukuliwa.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jayne Carney amesema kuwa walichukuwa hatua hiyo kuwalimda raia wake dhgidi ya magaidi hao ambao wameendelea kuwasaka.

Mbali na Mashariki na ya Kati na kaskazini mwa Afrika, Balozi za Marekani nchini Mauritiuys, Madagascar, Bunjumbura Burundi na Kigali Rwanda pia zimefungwa.