MAREKANI-YEMEN

UNHCR yasema imeimarisha usalama nchini Yemeni, Marekani yawaondoa wafanyakazi wake

Mseamaji wa UNHCR Melissa Fleming
Mseamaji wa UNHCR Melissa Fleming topnews.in

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa limeimarisha usalama nhcini Yemen wakati mataifa ya Magharibi yanafunga balozi zake nhcini humo kufuatia tahadhari ya tishio la ugaidi iliyotolewa na Marekani dunia nzima. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika hilo Melissa Fleming, amewaambia waandishi wa habari kuwa wao wapo nchini humo ingawa wanafanya shughuli zao kwa tahadhari kubwa na baadhi ya mipaka.

Aidha haikujulikana wazi kwamba hatua gani nyingine zitachukuliwa na taassisi mbalimbali za msaada za umoja wa mataifa UN katika kukabiliana na hofu hiyo ya mashambulizi.

Msemaji wa umoja wa mataifa mjini Geneva Corine Momal-Vanian amesema kuwa shirika hilo la dunia halikutoa maoni kuhusu hatua zake za kiusalama.

Washington imefunga baadhi ya balozi zake tangu siku ya Jumapili, nyingi kati ya hizo ni zilizopo katika mataifa ya Kiislamu, ikionya mashambulizi ya Al-Qaeda, na nchi za Magharibi zikafuata hatua za Marekani kwa kufunga balozi zake nchini Yemen.

Aidha Marekani leo Jumanne imewaagiza wamarekani waishio nchini Yemen kuondoka haraka iwezekanavyo na kuwaondoa wafanyakazi wake nchini humo.