SYRIA

Waasi takribani 62 wauwawa na wanajeshi wa serikali nchini Syria

Waasi wauwawa huko Damascus
Waasi wauwawa huko Damascus 62 Syria rebels dead in army ambush near Damascus

Wanajeshi wa serikali ya Syria wamewashambulia na kuwaua takribani waasi 62 katika shambulizi la kushtukiza leo Jumatano karibu na mji mkuu Damascus, Sirika la uangalizi wa haki za binadamu nchinih umo limearifu. 

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Syria limesema kuwa waliouwawa wengi wao wakiwa vijana ni wafuasi wa kundi la wanajihad la Al Nusra, huku nane wengine wakiwa hawajulikani walipo baada ya shambulio hilo lililotekelezwa majira ya alfajiri karibu na mji wa viwanda wa Adra Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu.

Chanzo kutoka jeshi la serikali kimekaririwa na shirika la habari la taifa SANA kikieleza kuwa jeshi limefanya shambulio la kushtukiza kwenye kundi la magaidi wa kundi la Al Nusra ambao walikuwa wakijaribu kupenyeza Mashariki mwa Ghuta na kushambulia kituo cha kijeshi.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa magaidi wote wameuwawa na silaha zao kukamatwa ingawa idadi haijatajwa.

Mji wa Adra ulioko umbali wa kilomita 35 kutoka mji mkuu Damascus, ni njia ya kuelekea Mashariki mwa Ghuta,ukanda wa kilimo ambako idadi kubwa ya waasi wanapatikana.

Mnamo Julai 21, waasi 49 waliuwawa katika mapigano baina yao na wanajeshi watiifu kwa serikali ya rais Bashar al Assad huko Adra.