MAREKANI

Marekani kufungua balozi zake zote siku ya Jumapili baada ya kutathimini upya tishio la Al Qaeda

Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki
Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki rfi

Marekani imesema kuwa, siku ya Jumapili itafungua upya balozi zake zote ambazo ilizilifunga juma hili isipokuwa moja iliyoko nchini Yemen, baada ya kutathmini upya tishio la Al-Qaeda. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Jen Psaki amesema Washington pia itaendelea kuufunga ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Lahore nchini Pakistan, baada ya kuwaondoa wafanyakazi wake siku ya Alhamisi.

Marekani ilikuwa imefunga baadhi ya balozi zake kwenye mataifa mbalimbali Afrika Kaskazini na Mashariki ya kati tangu Agosti 4 baada ya taarifa za kiinteligensia kuonya kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Qaeda.

Akizungumza mapema jan Ijumaa Rais Barack Obama, amesema kuwa Marekani inajaribu kuimarisha uwezo wa nchi katika kupambana na matawi ya ndani ya Al-Qaeda.