MISRI

Wafuasi wa Morsi wazusha vurugu zilizojeruhi watu kadhaa katika jimbo la Nile Delta

Mmoja wa wafuasi wa Morsi akiwa amebeba picha ya Mohamed Morsi
Mmoja wa wafuasi wa Morsi akiwa amebeba picha ya Mohamed Morsi REUTERS/Mohamed Abd El Ghany

Maelfu ya wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani na jeshi nchini Misri Mohamed Morsi wamekutana maeneo mbalimbali nchini humo na kuzusha vurugu ambazo zimesababisha watu kadhaa kujeruhiwa,huku Waziri Mkuu wa mpito akisema kuwa mwisho wa maandamano yao u karibu. 

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi hao wa Morsi walifurika kwenye mitaa katikati mwa jiji la Cairo na katika mji wa pili kwa ukubwa wa Aleksandria, wakiwa wamebeba picha ya kiongozi wao aliyeondolewa madarakani na kuimba nyimbo dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yalimwondosha Morsi mnamo Julai 3.

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchini humo MENA mapigano katika jimbo la Nile Delta kati ya waandamanaji wanaomuunga mkono Morsi na wakazi katika miji kadhaa, yamesababisha watu kadhaa kujeruhiwa,

Wafuasi wa Morsi ambao wamekuwa wakishikilia miji mikuu miwili kuu mbili wameapa kuendelea kupigana kwa ajili ya kurejeshwa madarakani kwa kiongozi wao, wakisema kwamba kupinduliwa kwake na jeshi Julai 3 ni ukiukwaji wa kanuni za kidemokrasia