Mali

Kura za uchaguzi zaendelea kuhesabiwa nchini Mali

Makasha ya kupigia kura yakiwa yamekusanywa tayari kwa kuhesabiwa
Makasha ya kupigia kura yakiwa yamekusanywa tayari kwa kuhesabiwa RFI/Laurent Correau

Zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa nchini Mali, limeanza hii leo baada ya kupiga kura za duru la pili mwishoni mwa juma lililopita zoezi linaloelezwa kuwa ni kufunguliwa kwa ukurasa npya baada ya nchi hiyo kuwa kwenye mgogoro wa kisiasa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Kinyanganyiro kikali ni kati ya Waziri Mkuu wa zamani Ibrahim Boubacar Keita na aliyekuwa Waziri wa fedha Soumaila Cisse .

Uchaguzi wa Mali unatarajiwa kuleta hali ya utulivu na uthabiti wa kisiasa nchini humo baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita.

Takriban wapigakura milioni saba walipiga kura mwishoni mwa juma lililopita, uchaguzi wa kwanza tangu mwaka 2007 ambao pia ni muhimu kwa ajili ya mustakabali wa uchumi wa Taifa la Mali

Waangalizi wa uchaguzi huo kutoka umoja wa ulaya wanatarajiwa kutoa Ripoti yenye kutathimini mwenendo wa uchaguzi hii leo.Waangalizi w Uchaguzi huo wanasema zoezi hilo lilikwenda vizuri.

Waangalizi huru wa uchaguzi takriban 2,000 walitoa tamko kuwa uchaguzi ulikuwa wenye utulivu lakini walieleza dosari za kuchelewa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura mjini Bamako na kusini mwa mji wa Koulikoro na Kayes.
 

Kwa upande wa Wagombea wa Urais Keita na Cisse kwa pamoja wamekuwa wakijiamini kushinda uchaguzi huo.
 

Kurejea kwa utawala wa kidemokrasia nchini Mali kutairuhusu ufaransa kuondoa vikosi vyao 4,500 walioingia nchini Mali mwezi Januari kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa kiislamu waliokuwa wamedhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya mapinduzi ya kijeshi.