Syria

Wanaharakati wa Upinzani waandaa mpango wa kuelekea maridhiano nchini Syria

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wakiwemo wanachama wa baraza la Muungano wa kitaifa wameandaa mpango wa kuelekea kufikiwa maridhiano na haki kwa Raia wa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo unatarajiwa kuwasilishwa siku ya jumatano, mbele ya Mkuu wa baraza la Muungano lakitaifa, Ahmed Jarba, lakini mpango huo bado haujaidhinishwa rasmi na makundi ya upinzani.
 

Hatua hiyo imekuja wakati kumekuwa na Ripoti kadhaa juu ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadam vinavyotekelezwa na Vikosi vya utawala na Wapiganaji waasi katika mgogoro wa Syria.
 

Ingawa maandamano ya nchini humo yalianza kwa amani mwezi Machi mwaka 2011 yaligeuka na kuambatana na Machafuko ambayo yamesababisha zaidi ya Watu 100,000 kupoteza maisha.
 

Waasi nchini Syria wamekuwa wakishutumiwa kukiuka kwa kiasi kikubwa haki za Binaadam vitendo vya kutesa watu na Mauaji.
 

Vikosi vya kijeshi, na makundi ya wanamgambo pia yamekuwa yakitupiwa shutma kama hizo.
 

Mapendekezo yaliyotolewa yanatoa wito wa kunyang'anya silaha na kulijenga upya kikosi cha usalama cha Syria na kuwang'oa Viongozi mafisadi.