SOMALIA

Chama cha Madaktari wasio na mipaka wasitisha Operesheni zao nchini Somalia

Wafakazi wa Shirika la Madaktari wasio na mipaka wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab
Wafakazi wa Shirika la Madaktari wasio na mipaka wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab REUTERS/Thomas Mukoya

Shirika la Madaktari wasio na mipaka wamefunga Operesheni zao nchini Somalia hii leo, wakieleza kuwepo kwa hali ya kuongezeka ukosefu wa usalama, baada ya kufanya kazi miaka 22 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Shirika hilo Unni Kurunakara amesema kusitishwa kwa operesheni yao ni matokeo ya kuwepo kwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wafanyakazi wa Shirika hilo, pia kutokana na mazingira ambayo Makundi ya Watu wenye silaha na Viongozi wa kiraia wamekuwa wakiendelea kuunga mkono, na kuendelea kupuuzia vitendo vya mauaji na utekaji nyara.
 

Kujiondoa kwa Shirika hilo na misaada yake ambayo shirika hilo lilijipatia sifa kufanya kazi kwenye mazingira mgumu na kuondoka kwa Shirika hilo kumeelezwa kuwa kutaathiri maelfu ya Raia wa Somalia.
 

Shirika la Madaktari wasio na mipaka limetibu watu zaidi ya 300,000 Mwaka huu pekee nchini Somalia.
 

Kurunakara ambaye amedai kuwa shughuli za Shirika lake zimekuwa hatarini ameeleza juu ya tukio la kuuawa kwa Wafanyakazi wake wawili mjini Mogadishu mwezi Desemba mwaka 2011 na kutekwa nyara kwa wafananyakazi Wawili wa Shirika hilo katika Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab ya nchini Kenya, Mwezi Oktoba mwaka 2011.
 

Karunakara amesema kuwa Mashambulizi yanayoendelea kushamiri nchini humo yamefanya Shirika hilo kuchukua uamuzi huo wenye kuumiza kwa kuwa hivi sasa nchini humo sheria za haki za binaadam haziheshimiwi.
 

Operesheni hiyo imefungwa katika maeneo 11, ikiwemo mogadishu, ambapo Shirika hilo lina kituo cha Watoto kwa kuwa maeneo mengi hayako chini ya Serikali za mitaa mfano Burao na Galkayo pia kusini mwa Kismayo.

Operesheni hizo pia zimesitishwa katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Wanamgambo wa Al Shabaab ambao waliruhusu shirika la Madaktari kufanya kazi ingawa walifukuza mashirika mengi ya misaada.