AFGHANISTANI-MAREKANI

Vikosi vya kigeni vilivyo Afghanistani vyatolewa wito kutangaza idadi ya Vikosi vitakavyobaki baada ya mwaka 2014

Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai REUTERS/Massoud Hossaini/Pool

Marekani na Washirika wake wametolewa wito kuwa watangaze ni Wanajeshi wangapi wataendelea kubaki nchini Afghanistani baada ya Mwaka 2014, kamanda wa zamani wa majeshi ya NATO James Stavrisis ameeleza.

Matangazo ya kibiashara

Stavridis ambaye amemaliza muda wake wa miaka minne akiwa kiongozi wa Majeshi ya NATO amesema ni muhimu kuweka wazi idadi ya Wanajeshi watakaobaki ili kufuta propaganda za kundi la Wanamgambo wa Taliban kuwa majeshi ya nchi za kigeni yanaitelekeza Afghanistani.
 

Kiongozi huyo wa Majeshi ya zamani amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Marekani na washirika wake kubakisha wanajeshi 15,000 nchini Afghanistani baada ya Wanajeshi wengine kuondoka nchini humo kabisa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014.
 

Hivi sasa kuna wanajeshi takriban 100,000 nchini Afghanistani chini ya Mwamvuli wa Majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi, NATO, huku Marekani ikiwa na takriban asilimia 60 ya Wanajeshi.
 

Maafisa wa Marekani walipendekeza kubakisha sehemu ndogo ya Jeshi lake nchini humo la Takriban vikosi 8,000 mpaka 12,000 baada ya Mwaka 2014.
 

lakini kutokana na kuwepo kwa hali ya kutoelewana kati ya Kabul na Marekani, Maafisa wa Ikulu ya Marekani walionelea kuwa wawaondoe wanajeshi wote wa Marekani baada ya mwaka 2014.