SYRIA

Kiongozi wa kundi la Hezbollah asema yuko tayari kupambana na wapinzani wa rais Assad nchini Syria

Kiongozi wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah
Kiongozi wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah theislamicnews.com

Kiongozi wa kundi la Hezbollah,Hassan Nasrallah amesema kuwa yuko tayari kupambana na Waislamu wenye msimamo mkali nchini Syria, siku moja baada ya shambulio baya la bomu kutokea huko Beirut. 

Matangazo ya kibiashara

Nasrallah pia amewashutumu waislam hao wenye msimamo mkali wa Sunni kwa kuhusika na shambulio la gari ambalo liliua takribani watu 22, baada ya kundi hapo awali kundi lisilojulikana kusema kuwa lilihusika na mashambulizi ya Alhamisi.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa endapo itamlazimu kufanya hivyo yuko tayari kwenda Syria yeye mwenyewe kupambana na waasi wanaopinga serikali ya rais Bashar al Assad.

Polisi wamesema takriban watu 22 waliuawa katika shambulio ambalo liliwalenga watu wengi waishio kusini mwa Beirut, na kujeruhi watu 325.

Hezbollah ni kundi muhimu linalomuunga mkono rais Bashar Al Assad na limepeleka wapiganaji kwenye eneo la mpakani na Syria mwaka huu kwa lengo la kuviongezea nguvu vikosi vya serikali ambavyo vimekuwa katika mapambano na wapinzani wa serikali tangu mwezi March mwaka 2011.