Syria-mapambano

Jeshi la Syria lashambulia ngome za waasi nchini humo.

Wanajeshi wa Syria
Wanajeshi wa Syria

Mapambano makali yameendelea kushuhudiwa nchini Syria katika mkoa wa pwani wa Attaquie uliopo magharibi mwa nchi hiyo ambapo jeshi limeshambulia kwa makombora na kumuuwa kiongozi mmoja wa kundi la wapiganji, shirika la haki za binadamu limethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limewatuma wanajeshi zaidi katika eneo hilo linalo aminika kuwa ndio kitovu cha rais Bashar Al Assad kupambana na wapiganaji walioweka kambi katika milima inayo inamia mji huo na ambao walianzisha mapambano takriban majuma mawili yaliopita
wakiwa hawana silaha za kutosha wapiganaji hao waliamuwa kujiunga na makundi ya wapiganai wa jihad wa makundi ya kiislam kutoka nchini Iraq licha ya uhusiano mbaya baina ya waasi na wapiganaji wa Makundi ya Jihad nchini Syria.

Mkuu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman amesema majeshi ya serikali ya serikali, yalimiminika kwa wingi katika eneo hilo la Attaquie kupambana na waasi na kufanya mashambulizi makali katika maeneo yaliokuwa yanashikiliwa na waasi.

Kituo cha televisheni ya taifa nchini Syria kimesema jeshi limefaanikiw akurejesha katika himaya yake miji iliokuwa inashikiliw ana makundi ya waasi katika jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na Kharata, Janzuriyeh, Baluta, Baruda na Hambushiyeh.

Hata hivyo Abdel Rahman, ameeleza kuwa mapigano hayo yalikuw amakali mno na kijeshi lilipata uwezo tu wa kudhibiti baadhi ya vijiji. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wapiganaji wengi wa makundi ya kigeni ya Jihad wameuawa katika mapigano hayo akiwemo kiongozi wa kundi la EIIL.

Kiongozi huyo wa kundi la EIIL aliuawa wakati wa mapigano katika kijiji cha Jamusiyeh
wakati huo huo jeshi la anga nchini Syria limeshambulia eneo la Jabal al Arbaine katika mkoa wa Edleb (kaskazini magharibi) mwa miji ya Daraya na Zabadani karibu na Damascus pamoja pia na mji wa Deir Ezzor mashariki mwa nchi hiyo
ngome ya waasi katika jiji la Homs imeshambuliwa pia na jeshi la serikali.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu laki moja wamepoteza maisha katika mapigano hayo ambayyo sasa yamedumu miezi 29. Jumamosi mwishoni mwa muma lililopita watu 124 wamepoteza maisha katika mapigano yaliojiri kwenye maeneo mbalimbali nchini humo.