AFRIKA KUSINI-MAHAKAMA

kesi ya bingwa wa mbio wa walemavu Oscar Pistorius dhidi ya mpenzi wake, kuamuliwa leo

Oscar Pistorius
Oscar Pistorius REUTERS/Siphiwe Sibeko

Bingwa wa mbio za walemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, ambaye anashtakiwa kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake katika siku ya wapendanao, amewasili mahakamani Jumatatu katika mahakama ambapo anatakiwa kuwepo mahakamani hapo kusikiliza mashtaka yanayomkabili.

Matangazo ya kibiashara

Vijana mwenye umri wa miaka 26ameingia katika chumba cha mahakama muda mfupi kabla ya moja na nusu majira ya kimataifa, akivalia koti na tai nyeusi pamoja na shati ya bluu, akiongozana na dada yake Aimee na kaka yake Carl, ambaye aliomba paomoja naye..

Wote watatu walipeana mkono, wakati Aimee yeye alikuwa akisoma maombi. Pistorius aliipa mgogo Camera huku akibubujikwa na machozi.

Kikao hicho mahakamani kinatakiwa kuwa kifupi mno. Jaji anaweza kuthibtisha kuwa kesi hiyo itasikilizwa mwezi March mwaka ujao kama alivyokuwa amefahamisha wakili wa Pistorius.

Mwanamichezo huyo analazima pia kusikiliza mashtaka dhidi yake baada ya kufikia mwisho wa uchunguzi, ambao matokeo yake yaliwasilishwa wiki iliyopita.

Jumatatu hii Agosti 19, mwanamitindo Reeva Steenkamp ingeliadhimisha miaka 30 kama asingelipigwa risase kadhaa na mpenzi wake Oscar Pistorius, Februari 14, siku ya Siku ya wapendanao.