KENYA-CHINA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, apokelewa kwa shangwe nchini China na mwenyeji wake Xi Jinping

Ma rais wa China Xi Jinping na Uhuru Kenyatta wa Kenya
Ma rais wa China Xi Jinping na Uhuru Kenyatta wa Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amepokelewa kwa shngwe na mwenyeji wake wa China Xi Jinping katika eneo la Tiananman ambako kikosi maalum cha walinzi walipelekwa katika eneo hilo kwa ajili ya kutowa heshima. Mizinga ishirini na moja ilirindima kwa ajili hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mapokezi viongozi hao walikutana kwa falagha katika jumba kuu la taifa.
Kenyatta alietawadhwa April baada ya kuibuka mshindi katika uchguzi mkuu uliofanyika tarehe nne march na ambaye anatuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kwa kuhusika kufadhili machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na ambapo kesi yake itasikilizwa Novemba 12 mwaka huu.

Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani zilionya kwamba wangeweza kupunguza mahusiano yao na kiongozi wa juu wa Kenya "mawasiliano muhimu", ingawa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alikutana na Rais wa Kenya jijini London kando na mkutano kuhusu Somalia uliofanyika nchini Uingereza.

Beijing kwa upande wake inasimama na sera yake ya kutoingilia katika masuala ya ndani ya nchi za Afrika, ambapo viongozi wake wanapongeza kukosekana kwa China, katika sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo.

China na Kenya ni washirika tangu mwaka 1960 wakati wa Uhuru ambapo China ilikomaza ushirikiano wake na mataifa ya Afrika katika kipindi hiki. China ni mshirika wa kwanza wa biashara na bara la Afrika.

China ikiwa maskini kwa maliasili, Kenya inachukuliwa na taifa hilo kubwa barani Asia kama mlango wa kuingilia katika bara la Afrika.

Nchi za Afrika ya Mashariki zinapewa kipaombele ya kimkakati na China, kuafuatia ukaribu wake na Serikali ya Sudani Kusini.