SADC-MKUTANO

Viongozi wa SADC waitaka Jumuiya ya kimataifa kuiondolea vikwazo Zimbabwe

Rais Robert Mugabe akiwa katika mkutano wa SADC
Rais Robert Mugabe akiwa katika mkutano wa SADC

Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi kusini wa Afrika SADC waliokutana huko Malawi katika mkutano wa sikiu mbili, wametowa wito kwa jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe baada ya kupasishwa kwa Robert Gabriel Mugabe katika uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC wametowa wito pia wa kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa dharura juu ya hali inayoendelea katika ukanda wa maziwa makuu na kukaribisha hali inayoendelea nchini Madagascar wakati ikikaribisha uchaguzi.

Katika mkutano wao wa mwaka viongozi wa SADC wameomba kuondolewa kwa aina yoyote ya vikwazo dhidi ya serikali ya Zimbabwe kwa mashirika na watu binafsi.

Kiongozi mpya wa SADC rais wa Malawi Joyce Banda amesema anaamini kwamba Zimbabwe na wananchi wake wametaabika sana na wanastahili kupumuwa kwa sasa.

Umoja wa Ulaya uliondowa baadhi ya vikwazo mwanzoni mwa mwaka huu vilivyokuwa vimewekwa tangu mwaka 2002 na ambavyo vilikuwa vinamlenga rais Mugabe na mashirika mawili. Marekani ilikuwa imeweka vikwazo mwezi March 2003 dhidi ya Mugabe pamoja pia na majina ya watu wa karibu yake.

SADC, imeipongeza Zimbabwe kwa kufaanikisha kuendesha uchaguzi katika hali tulivu na kumpongeza Mugabe na chama chake cha ZANU-PF kwa kujipatia ushindi wa kishindo.

Kwa kumthamini rais Mugabe viongozi hao wa SADC wamemteuwa Mugabe kuwa kaimu mwenyekiti wa kundi hilo na kuamuwa mkutano utaofuta wa mwaka 2014 ufanyike Julay nchini Zimbabwe.

Rais wa Botswana Ian Khama ambaye ambaye nchi yake ilikuwa imeomba kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya dosari zilizofuatia uteuzi wa rais Mugabe amekutana na rais huyo wakati wa mkutano huo.

Mugabe wenye umri wa miaka 89 ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa kuliko wote barani Afrika na anaelekea kuanza muhula wake wa saba wa kipindi cha miaka 5, aliingia madarakani tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake mwaka 1980.

Shughuli za kuapishwa kwa kiongozi huyo zinataji kufanyika alhamisi juma hili, msemaji wake George Charamba amethibitisha jana akiwa jijini Lilongwe.
Mpinzani wake mkuu waziri mkuu Morgan Tsvangira aliondowa kesi kupinfga matokeo ya uchaguzi siku ya Ijumaa baada ya kuona kwamba kesi hiyo itakuw ana upendeleo.