SYRIA-LEBANON

baraza la ushirikiano la nchi za ghuba la laani vikali kauli ya kiongozi wa Hezbollah kupelekea wapiganaji zaidi nchini Syria

Baraza la Ushirikiano la nchi za ghuba ya kiarabu, limeituhumu vikli kauli ya kutowajibika iliotolewa na kiongozi wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon Hassan Nasrallah ambaye ametishia kupeleka wapiganaji zaidi wa Hezbollah nchini Syria baada ya mashambulizi dhidi ya ngome yake nchini Lebanon.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la ushirikiano la nchi za huba limesema, Wakati baadhi ya nchi ulimwenguni zinalaani ushiriki wa wanamgambo wa kundi la Hezbollah katika mapigano nchini Syria, Nasrallah anatishia kushirikisha zaidi wapiganaji wake katika mapigano yanayoendelea nchini Syria, na huu ni uingiliaji dhahiri katika maswala ya ndani ya syria.

Katibu Mkuu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, alisema katika sala ya Ijumaa juma lililopita kwamba yupo tayari kwenda kupambana nchini Syria na kupeleka wapiganaji zaidi ya kusaidia serikali ya kupambana na Waislamu wenye msimamo mkali wanaotuhumiwa kuhusika katika mashambulizi dhidi ya ngome zake katika Lebanon.

Watu ishirini na saba waliuawa katika shambulio hilo Alhamisi kwamba katika shambulio lililotikisa kusini mwa jiji la Beirut kuliko ngome ya Hezbollah, lenye nguvu ya kijeshi na ambalo linashiriki kuisaidia serikali ya Syria ya Bashar al-Assad kupambana na waasi.

Baraza la ushirikiano la nchi za ghuba GCC linalo jumuisha nchi za Bahrein, Kuweit, Oman, Qatar, Saudi Arabia, na Falme za Kiarabu, liliamuwa kuweka vikwazo dhidi ya wanachama wa Hezbollah wanaoishi katika nchi wanachama wa baraza hilo kufuatia hatuwa ya kundi hilo kutowa msaada wa kijehi kwa serikali ya Syria.