MISRI-MACHAFUKO

Kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Biradherhood Mohamed Badie akamatwa wakati machafuko yakiendelea

Kiongozi mkuu wa Muslim Bradherhood Mohamed Badie
Kiongozi mkuu wa Muslim Bradherhood Mohamed Badie

Mapambano dhidi ya wafuasi wa chama cha muslim Bradherhood nchini Misri yanaendelea, huku polisi ikimtia nguvunu kiongzi mkuu wa chama hicho Mohamed Badie wakati takwimu za machafuko zikionyesha watu mia tisa ndio ambao wamepoteza maisha katika nchi nzima tangu Jumanne Juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Mohamed Badie kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa wafuasi wa rais aliepinduliwa madarakani Mohamed Morsi, amekamatwa katika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne akiwa pamoja na viongozi wengine wawili wa ngazi ya juu wa chama hicho wakiwa katika majengo yaliokaribu na eneo la Rabaa al Adawiya eneo ambalo watu 280 walipoteza maisha wakati polisi ilipoanza kuwashambulia waandamanaji.

Televisheni ya taifa na binafsi nchini Misri zinaunga mkono pakubwa hatuwa ya jeshi kuuangusha utawala wa rais Morsi, zimeonyesha picha za Mohamed Badie mwenye umri wa miaka 70 alivo kamatwa na polisi.

Vyombo vya sheria nchini humo vilikuwa vimeamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo pamoja na viongozi wengine wa chama cha Muslim Bradherhood kwa tuhumu za kuchochea machafuko tangu Jualy 10 tangu kuangushwa kwa Mohamed Morsi, rais wa kwanza wa taifa hilo aliyekuwa amechaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia.

Licha ya lawama zinazo tolewa kutoka jamii ya kimataifa, serikali iliowekwa madarakani na jeshi nchini humo imeamuru kuwasambaratisha waandamanaji wa chama cha muslim Bradherhood, hali ambayo inayosababnisha umwagaji mkubwa wa damu.

Takriban watu mia tisa wanakadiriwa kupoteza maisha tangu siku ya Jumatano wakati jeshi lilipo vamia eneo la Rabaa na kuwauawa wafuasi wa rais Morsi ambao walikuwa wakiandamana.

Utawala uliopo, umewaruhusu polisi na jeshi kuwashambulia kwa risase waandamanaji. Hapo siku ya jumapili, Kiongozi wa jeshi jenerali Abdel Fatah al-Sissi alisema, nchi yake haitorudi nyuma mbele ya “magaidi” ambapo utawala uliopo na vyombo vya habari vinawachukulia wafuasi wa Muslim Bradherhood kama magaidi.

Ma elfu ya wafuasi wa Mohamed Morsi wametiwa nguvuni na ambapo wanatarajiwa kupandishwa kizimbani Agosti 25, akiwemo Mohamed Badie.

Mtoto wa kiongozi huyo, alikuwa miongoni mwa watu waliouawa kwa risase siku ya ijumaa juma lililopita jijini Cairo.