MAREKANI-ZIMBABWE

Marekani yasema, ipo tayari kuondowa vikwazo kwa Zimbabwe iwapo rais Mugabe atafanya mabadiliko kwa mujibu wa matakwa ya wananchi

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jennifer Psaki
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jennifer Psaki

Serikali ya Marekani imesema itaondowa vikwazo kwa Zimbabwe iwapo rais wa nchi hiyo Robert Gabriel Mugabe atafanya mageuzi kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wa taifa lake. Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC katika kikao chao juzi Jumalili nchini Malawi, walitowa wito kwa mataifa ya magharibi kuondowa vikwazo dhidi ya serikali ya Zimbabwe baada ya kuidhinisha uchaguzi uliompa nafasi Rais Robert Gabriel Mugabe kuendelea kuliongoza taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jennifer Psaki amesema walisema wazi kwa serikali ya Zimbabwe na ukanda mzima kwamba mabadiliko ya sera za vikwazo ya Marekani itaingilia kati wakati serikali ya Zimbabwe itapo fanya mabadiliko ya wazi kwa kufuata matakwa ya wananchi.

Msemaji huyo wa serikali ya Marekani amesema kuna uwezekano wa kuondolea vikwazo Zimbabwe, lakini mpango wa Marekani wa vikwazo vya malengo utabaki kwa kwa muda wote kutakuwa hakuna mabadiliko.

Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC waliomba kuiondolea kila aina ya vikwazo serikali ya Zimbabwe wakati wa kutamatisha kikao chao cha kila mwaka kilicho fanyika nchini Malawi.

Umoja wa Ulaya ulisitisha sehemu ya vikwazo kwa serikali ya Zimbabwe vilivyowekwa mwaka 2002 na ambavyo viliwalenga watu 10 washirika wa karibu na Mugabe akiwemo pia rais Robert Gabriel Mugabe. Marekani ilimuwekea vikwazo rais Mugabe mwaka 2003 pamoja pia na orodha nyingine ya watu wa karibu na kiopngozi huyo.