PAKISTAN

Rais wa zamani wa Pakistan Pervez Musharaf afunguliwa mashataka rasmi ya mauaji dhidi ya mwanasiasa Benazir Bhutto

Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Mushar wakati akiwasili mahakamani mwei wa April mwaka huu
Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Mushar wakati akiwasili mahakamani mwei wa April mwaka huu

Rais wa zamani wa Pakistan Pervez Musharraf ameshtakiwa rasmi Jumanne hii kwa Makosa ya mauaji ya mpinzani wake wa zamani Benazir Bhutto, ambaye aliuawa mwaka 2007 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkuu wa zamani wa jeshi nchini Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

Muendesha mashtaka mkuu nchini humo Chandhry Azhar amesema, baada ya kusikilizwa kesi hiyo katika mahakama ya kupambana na ugaidi mjini Rawalpindi, mji jirani na islamabad, kwamba Pervaz Musharaf anashtakiwa kwa mauaji, jinai kula njama za kufanya mauaji na kurahisisha mauji ya Benazir Bhutto,

Musharraf Pervez anakabiliwa na matukio kadhaa, tangu kurejea Pakistan mwishoni mwa mwezi Machi baada ya miaka minne ya uhamisho kati ya Dubai na London, ikiwa ni pamoja na mauaji ya Bhutto.

Jenerali huyo wa zamani anaezuiliwa nyumbani kwake karibu na mji mkuu wa Islamabad, amefikishwa Jumanne hii mahakamani akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na vikosi maalum. Kulingana na mpigapicha wa shirika la habari la AFP, barabara za mji huo zimefungwa.

Muendesha mashtaka amesema Mashitaka yamesomwa huku mshtakiwa akikana tuhuma zote dhidi yake na kuongeza kuwa kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena wiki ijayo.

mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha Pakistan Peoples Party (PPP) aliye uawawa Desemba 27, 2007 mbele ya maelfu ya wafuasi katika mji wa Rawalpindi wakati wa mashambulizi ya silaha ndogo iliofutiwa na shambulio la kuvizia, bado ni mauaji ya ajabu katika historia ya Pakistan.

Wakili wa musharaf Sayeda Afshan Adil amesema Madai dhidi ya mteja wake hayana msingi na hawana hofu yoyote, watafuta tu utaratibu na kuheshimu mchakato wa mahakama.