Lebanon-Israeli

Ndege za Israeli zimeshambulia ngome ya wapiganaji wa kigaidi kusini mwa mji mkuu Lebanon

Ndege za Israeli zikilenga mashambulizi ya ngome za wapiganaji wa makundi ya kiislam kusini mwa lebanon
Ndege za Israeli zikilenga mashambulizi ya ngome za wapiganaji wa makundi ya kiislam kusini mwa lebanon

Ndege za Israel zimeshambulia maeneo ya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa kile msemaji wa jeshi hilo anadai yalilenga ngome za makundi ya kigaidi kwenye eneo la Na'ameh, ikiwa ni jibu kwa shambulio lililotokea saa chache katika ardhi ya Israeli, baada ya kundi hilo kukiri kuhusika.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya makombora manne yalirushwa kwenye ardhi ya Lebanon yakilenga ngome muhimu ya kundi la FPLM-CG linalo ongozwa naAhmad Jibril nchini humo ambalo wapiganaji wake wanaisaidia serikali ya rais Bashar al-Assad.

Shambulio hili linatekelezwa ikiwa imepita siku moja toka kurushwa kwa kombora lililotua kwenye ardhi ya Israel kutokea nchini Lebanon, hakuna taarifa za watu kuuawa ama kujeruhiwa.

Msemaji wa kundi hilo Ramez Moustapha, amesema kwamba ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia eneo la Na'ameh bila kusababisha madhara yoyote. Hata hivyo memjai wa kundi hilo amekaniusha taarifa za kundi hilo kuhjusika katika amshambulizi ya roketi ya hivi karibuni dhidi ya utawala wa Israel.

Kundi la FPLP-CG halihusiki na shambulio lolote la Reketi, ameendelea kusema Ramez Moustapha na kuongeza kuwa kuna maswali ya kuhoji kuhusu muda unaotolewa juu ya kurushwa kwa roketi hizo, na kuongeza kuwa Israel inafanya mbinu za kuwagawa wapalestina na wa Lewbanon.

Awali jeshi la Israel lilifahamisha katika taarifa yake kwamba jeshi lake la anga limeedesha mashambulizi ya roketi nchini Lebanon muda mchache baada ya kutokea mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Israel yaliotekeleza na kundi lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda baada ya kundi hilo kukiri kuhusika.