SUDANI KUSINI

Raisi wa Sudan Kusini Salva Kiir amteua kiongozi wa zamani wa waasi kuwa makamu wake

Raisi wa Sudan Kusini Salva Kiir
Raisi wa Sudan Kusini Salva Kiir rfi

Raisi wa Sudani Kusini Salva kiir amemteua kiongozi wa zamani wa waasi James Wani Iga kuwa makamu wake,vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimearifu.

Matangazo ya kibiashara

Igga, ambaye amekuwa spika wa bunge la Sudan kusini tangu 2005 ameonekana kuwa chaguo linalosawazisha tofauti ya kikabila kati ya viongozi wa taifa na itasaidia sana hali ya mambo kuelekea uchaguzi mwaka 2015.

Igga ambaye ni Naibu mwenyekiti wa chama cha SPLM anatokea katika kabila la Bari ambao ni wenyeji wa eneo la Juba.

Mwezi uliopita raisi Kiir alichukua hatua ya kushangaza baada ya kuvunja Baraza la Mawaziri na kisha kumfuta kazi Makamu wa Rais Riek Machar kitu kilichotajwa kuchangiwa na tofauti za kisiasa baina yao.

Makamu mpya wa Rais Kiir anatarajiwa kushauriana naye kuunda Baraza jipya la Mawaziri.