SYRIA

Marekani na Uingereza zimesema ishara zaidi zaonesha kuhusika kwa serikali ya Syria katika mashambulizi ya silaha za kemikali dhidi ya watu wake

Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron the sun.co.uk

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wamekuwa karibu jana Jumamosi katika kulaumu vikosi vya serikali ya rais bashar al Assad kwa mashambulizi makubwa ya silaha za kemikali karibu na mji wa Damascus. 

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa Marekani na Uingereza kwa pamoja wameguswa na kuongezeka kwa ishara kwamba hilo lilikuwa shambulizi kubwa la kemikali lililofanywa na vikosi vya serikali dhidi ya watu wake.

Ukweli kwamba Rais Assad imeshindwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa unaonyesha kwamba serikali ina jambo la kuficha,zimeongeza taarifa hizo na kubainisha kuwa matumizi hayo ya silaha za kemikali yanastahili mwitikio mkubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Wakati huo huo serikali ya Syria na washirika wake wametuhumiana wao kwa wao kwa kutumia silaha za kemikali wakati madaktari wasio na mipaka kusema kuwa watu 355 wamepoteza maisha kutokana na dalili za sumu ya neurotoxic huku maelfu wengine wakipatiwa matibabu hospitalini.