CHINA

Kesi ya mwanasiasa wa China Bo Xilai yakamilika

 Kesi ya ufisadi na utumizi mbaya wa mamlaka inayomkabili mwanasiasa mashuhuri wa China Bo Xilai imakamilika.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Mashtaka wamewaambia Majaji kuwa mwanasiasa huyo hastahili kupewa msamaha au kuonewa huruma wakati hukumu itakapokuwa inatolewa kutokana na uzito wa makosa aliyoyafanya.

Wakati kesi hiyo ikimaliza Xilai aliyewahi kuwa kiongozi wa chama cha Kikomunisti ameendelea kusisitiza kuwa hakuhusika kwa vyovyote vile na ufisadi, na matumizi mabaya ya mamlaka kama anavyotuhumiwa.

Aidha, Xilai amesema kuwa mlinzi wake aliamua kuacha kazi baada ya kugundua kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake Gu Kailai.

Kesi hiyo imemalizka baada ya kusikilizwa kwa siku tano na haijabainika ni lini uamuzi utatolewa.

Mwanasiasa huyo na mke wake pia wanatuhumiwa kupanga kifo cha mafanyibiashara maarufu na  raia wa Uingereza Neil Heywood mwaka 2012 tuhma ambazo pia amezikanusha.

Hii ndio kesi kubwa ya kisiasa kuwahi kufanyika nchini China kwa kipindi kirefu dhidi ya mwanasiasa mashuhuri na wachambuzi wa siasa wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa Bo Xilai mwenye umri wa miaka 64 akapatikana na hatia na kufungwa jela.

Bo Xilai alihudumu wakati mmoja kama Waziri wa biashara, pia alikuwa Meya wa mji wa Dalian na kuhudumu kama Katibu wa chama cha Kikomunisti.