RWAND-DRC

Rwanda yakanusha kuwa inapanga kuishambulia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

REUTERS/James Akena

Nchi ya Rwanda imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wapo tayari kupambana na majirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, taarifa hizo zilienea baada ya kushuhudiwa msafara wa wanajeshi na magari ya silaha kutokea mjini Kigali kuelekea eneo la mpakani na DRCongo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa nchi za nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema vikosi vya nchi yake havijaingia DRC na andapo uamuzi huo utachukuliwa basi taarifa zitawekwa wazi, taarifa hiyo ameitoa kupitia mtandai wa kijamii wa twitter.

Hayo yanakuja wakati mapigano yaliyoshuhudiwa hivi karibuni baina ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali ya DRC yakisitishwa na waasi kusema wamerudi nyuma umbali wa kilomita tano kutoka eneo la mapigano.

M23 wanasema wamefikia uamuzi huo ili kuruhusu uchunguzi ufanyike na kubaini ni nani aliyerusha bomu katika nchi jirani ya Rwanda tukio ambalo lilisababisha kifo cha mama mmoja na kujeruhiwa kwa mtoto wake.

Jeshi la serikali FRDC wakishirikiana na vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani nchini DRCongo na upande wa pili wa waasi wa M23 wamekuwa wakishutumiana kila mmoja akimtaja mwenzie kuhusika na shambulizi hilo.