DRCONGO-MONUSCO-M23

Marry Robinson atua Kinshasa, M23 wataka mazungumzo

AFP PHOTO/JUSTIN TALLIS

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu Bi. Marry Robinson amewasili jana jijini Kinshasa na kupokelewa na mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja huo Martin Kobler.

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara Marry Robinson analenga kuangalia hali ya mambo nchini DRC kufuatia mapambano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo ambapo pia kiongozi huyo atatembelea nchi za Rwanda na Uganda.

Robinson leo anatembelea mji wa Goma mashriki mwa DRCongo ambako atakutana na viongozi wa Mkoa huo na viongozi wa mashirika ya kiraia, kabla ya kurejea jijini Kinshasa hapo Kesho ambako atakutana na viongozi wa taifa hilo naa baadaye kuelekea jijini Kampala na Kigali

Ziara hiyo inakuja siku chache baada ya kushuhudiwa mapigano makali baina ya waasi wa M23 na majeshi ya serikali ya FARDC yakisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa na FARDC vilifaulu kuwasambaratisha waasi baada ya kuvurumisha makombora katika jiji la Goma yaliosababisha mauaji ya raia wasiokuwa na hatia.

Kiongozi wa waasi wa M23 aliyekuwa katika majadiliano ya Kampala Kambaso Ngueve anaituhumu serikali ya DRCongo kwa kushindwa kuendeleza majadiliano ya kampala na kwamba njia pekee ya mzozo huo ni mazungumzo.