SYRIA-MAREKANI-G20

Maseneta wa Marekani waridhia Syria kushambuliwa, Obama kushawishi G20 kuchukua hatua

Jopo la maseneta wa Marekani limeridhia maazimio ya kuingilia kijeshi nchini Syria baada ya kubainika majeshi ya raisi wa syria basharl alAssad yanajihussha na mashambulizi ya silaha za kemikali dhidi ya waaasi.

REUTERS/Jonas Ekstromer/Scanpix Sweden
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry  ameendelea kuwahimiza maseneta kuwa suala la kuingilia kijeshi nchini syria halieukiki na kutokuchukua hatua hiyo ni kujihatarishia usalama zaidi.

Naye Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa UN Ban Ki-moon amesema ataendelea kushinikiza kupatikana kwa suluhu ya kisiasa nchini Syria ambako mzozo huo umeendelea kusababisha maafa ya zaidi ya watu laki moja.

Ban Ki Moon ameyasema hayo akiwa katika chuo kikuu kilichopo mjini saint Petersburg huko Urusi kabla ya kuhudhuria mkutano wa mataifa tajiri kiviwanda duniani maarufu kama G20 ambao unaanza alhamisi hii.

Ban amesema haki za binadamu ziko hatarini na demokrasia imeendelea kutishika wakati harakati mbalimbali za kupata suluhu zikikabiliwa na upinzani mkali.

Kwa upande wake Rais Barack Obama wa Marekani ameendelea kutafuta uungwaji mkono wa kimataifa kuhusu maazimio yake kuingilia kijeshi nchini syria akieleza kwamba sheria za kimataifa ni muhimu.

Akiwa nchini Urusi ambako mkutano wa mataifa tajiri kiviwanda maarufu kama G20 unaanza hii leo Obama amesema kuwa Utawala wa Syria umevuka mipaka na anatarajia kuwashawishi viongozi wa mataifa hayo kuchukua hatua dhidi ya Syria.