SYRIA-MAREKANI

Bunge la Syria lawataka wabunge wa Congress nchini Marekani kugomea ombi la Rais Obama

Bunge la Syria limelitaka Bunge la Congress nchini Marekani kutoridhia hatua inayotaka kutekelezwa na Serikali ya Barack Obama ya kuishambulia kijeshi nchi hiyo.

REUTERS/SANA/Handout
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Obma inataka Syria ishambuliwe kijeshi kutokana na tuhuma za kutumia silaha za kemikali na kuangamiza raia wasio na hatia.

Bunge la Congress nchini Marekani linatarajia kuketi wiki ijayo kujadili pendekezo lililowekwa mezani na Rais Barack Obama akitaka hatua hiyo itekelezwe ili kumwadabisha Rais Bashar Al Assad.

Mkuu wa Bunge la Syria amewataka wabunge wa Congress kutumia uwezo wao kuzuia Marekani kuingia vitani kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa syria.

Amesema kuwa Marekani kwa kutumia nafasi yake bado inawezan kutumia njia za kidiplomasia badala ya kukimbilia vita ambayo madhara yake yatakuwa makubwa.

Bunge la Syria limetuma ujumbe huo kwa wajumbe wa Congress nchini Marekani kupinga pendekezo la Rais Barack Obama.