SYRIA

Kerry kusaka uungwaji mkono kuhusu Syria kwenye mkutano na mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry REUTERS/Jason Reed

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry leo Jumamosi huenda akaanza harakati za kutafuta kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya kuhusu kuingilia kijeshi nchini Syria baada ya mkutano wa Mataifa yenye nguvu za kiviwanda duniani, G20 kushindwa kutatua mgawanyiko mkali baina ya Washington na Moscow. 

Matangazo ya kibiashara

Kerry atashinikiza hatua ya adhabu dhidi ya Syria baada ya kile ambacho Marekani inasema serikali ya rais Bashar ala Assad ilitumia silaha za kemikali katika mashambulizi karibu na Damascus, licha ya mgawanyiko wa kina kuhusu suala hilo miongoni mwa mataifa yenye nguvu duniani.

Jana Ijumaa, Rais wa Marekani Barack Obama na rais wa Urusi Vladimir Putin walishindwa kutatua tofauti zao katika mkutano wa kilele wa G20 huko Saint Petersburg huku nusu ya wajumbe wa mkutano huo wakitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya madai ya mashambulizi ya kemikali huko Damascus mwezi uliopita.

Kery atafanya mkutano na mawaziri wa kigeni 28 wa umoja huo huko Lithuana ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya uenyekiti wa umoja huo.