Marekani na Urusi zakubaliana kuondoa silaha za kemikali nchini Syria kufikia katikati ya mwaka 2014
Marekani na Urusi zimezindua mpango kabambe wa kuondoa silaha za kemikali nchini Syria hadi kufikia katikati ya mwaka 2014, hivyo kuzua mchakato wa kidiplomasia leo Jumapili ili kupata uungwaji mkono wa kina wa kimataifa katika mpango huo.
Imechapishwa:
Makubaliano hayo ya kihistoria, yaliyotangazwa mjini Geneva jana Jumamosi, yaliacha mlango wazi kwa vikwazo ambavyo havikubainishwa ikiwa Damascus itashindwa kuzingatia, na makubaliano hayo yalipongezwa haraka na mataifa ya Magharibi.
Hata hivyo mpango huo vile vile ulikataliwa kwa haraka na waasi wa Syria ambao walionya kuwa mpango huo hautasitisha umwagaji damu katika machafuko ambayo yamegharimu maisha ya watu zaidi ya laki moja na kusababisha wengine kukosa makazi katika kipindi cha miaka miwili na nusu.
Chini ya mkataba huo uliojadiliwa kwa siku tatu za mazungumzo mjini Geneva kati ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na cheo mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov, Rais wa Syria Bashar al-Assad sasa amepewa juma moja kuwasilisha maelezo ya hifadhi ya serikali yake.