DRCongo-Rwanda

SADC yaonesha wasiwasi kuhusu ongezeko la askari wa Rwanda kwenye mpaka wa DRC

Wajumbe wa SADC mkutanoni
Wajumbe wa SADC mkutanoni dailynews.co.tz

Taarifa kutoka kwenye bodi ya kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeeleza kuwa na wasiwasi kutokana na kupelekwa kwa askari wa Rwanda kwenye mpaka wa kawaida na kwamba bodi hiyo inamatumaini kuwa Rwanda haifikirii kuvamia DRC.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo Iliyotolewa jana kwenye mkutano wa kilele wa SADC nchini Namibia na kuhudhuriwa na Rais wa DRC Joseph Kabila,imezitaka nchi jirani kuchangia harakati za kuleta amani , usalama na utulivu nchini DRC.

Askari wa DRC wakisaidiwa na kikosi maalumu cha askari wa umoja wa mataifa UN walianzisha mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa M23 mwezi uliopita katika eneo la Mashariki mwa DRC.

SADC pia ilivipongeza vikosi vya askari wa serikali ya DRC na kikosi maalum cha umoja wa mataifa UN kwa kuendelea kutoa shinikizo la kijeshi kwa waasi wa M23 na makundi hasi mengine mMashariki mwa DRC