DRCongo- Rwanda

Hali tete katika mpaka wa DRCongo na Rwanda baada ya askari mmoja wa FARDC kutekwa na polisi wa Rwanda

Jeshi la nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo limeshutumu vikosi vya Rwanda kuvuka mpaka siku ya Jumapili na kumteka nyara mmoja wa maafisa wake wa kijeshi, mashariki mwa nchi hiyo. Duru za Kijeshi zinasema kwamba Sargenti Mulanga Kusakala ambaye alikuwa ametembelea familia yake na wakati akitembea katika eneo lisilo kuw ana mwenyewe kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili ndipo askari polisi watatu wa Rwanda walimteka na kumpeleka nchini Rwanda.

Gisenyi nchini Rwanda katika eneo la mpaka na FARDC
Gisenyi nchini Rwanda katika eneo la mpaka na FARDC
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi la Congo jimboni kivu ya kaskazini Olivier Hamuli amesema tukio hilo ni la utekaji nyara kwa kuwa Mwanajeshi huyo alikuwa kwenye ardhi ya nchi yake na si nchini Rwanda, na taarifa hiyo ya kutekwa kwa mwanajeshi huyo ilitolewa na wananchi baada ya hali kuonekana kuwa mbaya ambapo amsema wamelazimika kupunguza ghadhabu ya wananchi waliokuwa na hasira ambao waliandamana kwenye mpaka baina ya Rwanda na DRCongo.

Maandamano hayo yalisababisha mipaka yote kufungwa kwa muda kabla ya kufunguliwa tena baada ya ghadhabu ya wananchi kupungua ili kuruhusu watu kureja nyumbani kutoka kila upande.

kwa mujibu wa mashahidi kutoka Goma, hali bado ni tete katika eneo hilo la mpaka, kwani wananchi wengi walikuwa bado ni wengi katika eneo la mpaka ambapo baadae jioni wanajeshi wa DRCongo na polisi walimiminika kwa wingi katika eneo hilo.

Kulingana na msemaji wa jeshi la DRCongo FARDC, Olivier Hamuli, Sergenti Mulanga Kusakala ni mwenye asili ya Mkoa wa Bandundu magharibi mwa Congo na anatumikia katika kanda ya kumi ya kijeshi katika mji wa Bukavu, mki mkuu wa Mkoa wa Kivu ya Kusini.

Mamlaka ya Rwanda imesema kuwa wamemkamata mwanajeshi wa congo aliyekuwa na Silaha nzito katika ardhi yao wakati Wanajeshi wa Rwanda walipokuwa wakifanya doria mjini Rubavu mji unaotenganisha nchi hizo mbili.

 Uhusiano kati ya Rwanda na DRCongo umekuwa mbovu tangu mwezi Mei 2012 wakati waasi wa kundi la M23 walipoanza uasi dhidi ya serikali na ambapo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakizilaumu Rwanda na Uganda kuwaunga mkono waasi hao, jambo ambalo nchi hizo zimekuwa zikikanusha.