Soka-fifa

Kiongozi wa shirikisho la soka nchini Australia aitaka FIFA kufanya maamuzi sahihi kuhusu kuandaa kombe la dunia la mwaka 2022 nchini Qatar

Kiongozi wa shirikisho la soka nchini Australia
Kiongozi wa shirikisho la soka nchini Australia news.com

Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Australia Frank Lowy ameitolea wito shirikisho la soka duniani Fifa kufanya mashauriano kwanza kabla ya kuchukuwa uamuzi wowote wa kupanga rabiba michuano ya duniani katika msimu wa majira ya baridi nchini Qatar mwaka 2022.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo amebaini kuwa FIFA sasa ina nafasi ya kufanya maamuzi sahihi katika kuandaa mikakati ilio wazi na kwa mpangilio, tofauti na mchakato ambao ulisababisha uamuzi mbaya katika mwezi Desemba mwaka 2010.

FIFA ilitowa maamuzi ya kutatanisha mwaka 2010 ya kuamuru michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 yafanyika nchini Qatar, ambapo Australia nayo ilikuwa inawania.

Michel Platini rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA amekuwa akipendekeza mara kadhaa michuano hiyo ifanyika katika majira ya bairidi ili kuepuka majira ya joto ambayo hufikia hadi kwenye nyuzi 50 nchini Qatar katika kipindi hicho, jambo ambalo ni hatari sana kwa wachezaji lakini pia kwa mashabiki.

Tarehe 18 Julai, mkuu wa FIFA Sepp Blatter pia alitetea msimamo huu, baada ya muda mrefu na kuamini kwamba ombi hili linatakiwa kutolewa na nchi mwenyeji wa michuano hiyo.

Bosi wa soka nchini Australia amefahamisha kwamba iwapo ratiba hiyo ya Dunia-2022 itafanyika katika majira ya baridi, basi itolewe fidia kwa mgombea aliyeshindwa wakati wa mchuano 2022 ambaye alikuwa amepanga kuandaa michuano hiyo katika miezi ya Juni na Julai.