Somalia-EU

Somalia yakubaliwa kupewa msaada wa Euro bilioni 1.8 kutoka Jumuiya ya Kimataifa

Jumuiya ya kimataifa imeahidi kutowa msaada kwa serikali ya Somalia unaofikia Euro Bilioni 1.8, utaosaidia kuijenga upya nchi hiyo ilioganwanyika vipande kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo sababisha mauaji makubwa na kuwaacha raia wengi katika hali ya umaskini usiokuw ana kifani.

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud na kiongozi wa EU Manuel Barroso
Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud na kiongozi wa EU Manuel Barroso
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso amesema jana katika mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia uliofanyika jijini Brusels Ubelgiji, wapo tayari kutolea Somalia msaada wa Euro Bilioni 1.8 ikiw ani mara mbili zaidi ya kiel ambacho Umoja wa Ulaya ulitaji kutowa kwa Somalia.

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud amesema ni siku ya kihistoria kwa Somalia.

Umoja wa Ulaya uliahidi kutowa Euro Miloni 650, ukifuatiwa na Sweden, Danmark Ujerumani na Uingereza. Tangu mwaka 2008, Umoja wa Ulaya tayari umekwisha itolea msaada nchi ya Somalia wa Euro Bilioni 1.2.

Manuel Barroso amesema fedha hizo zitasaidia katika ujenzi wa taifa hilo baada ya kukumbwa na vita kwa takriban miaka ishirini sasa na kusaidia kuandaa uchaguzi wa mwaka 2016.

Rais wa Somalia ameutaka Umoja wa Ulaya kutekeleza ahadi zake ili kuisaidia Somalia kujikwamua kutoka katika lindi la machafuko, amesisitiza kuwa, itategemea jinsi utaratibu utawekwa ili kuhakikisha utoaji wa fedha hizo.

Amesisitiza kuwa mpango wa ujenzi uiolipitishwa wakati wa mkutano utaisadia Somalia kupiga hatuwa kubwa ya mandeleo." Lengo ni kuandaa ahueni chini ya misingi minne itayopewa kipao mbele: usalama, mageuzi ya mahakama, mageuzi ya fedha na kufufua uchumi.

Katika Kuhakikisha kuendelea kutowa msaada wa washirika wa kimataifa, mwakilishi wa EU, balozi Catherine Ashton, alibainisha kuwa orodha ya mahitaji ni ndefu mno huku kukiwa na changamoto kubwa. Kujenga ajira ili kuzuia kuibuka kwa vitendo vya uharamia, ambavyo vimekuwa vikivuruga ghughuli za baharini katika pwani ya Somalia, ni moja miongoni mwa malengo, alisema Barroso.