Zimbabwe-EU

Umoja wa Ulaya waondowa vikwazo kwa makampuni nchini Zimbabwe wakati rais Mugabe akionya kuendeleza sera yake ya kuwapa nafasi wazawa wa taifa hilo.

Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe Agosti 25 jijini Harare
Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe Agosti 25 jijini Harare REUTERS/Philimon Bulawayo

Umoja wa ulaya EU umeanza taratibu za kuondoa vikwazo dhidi ya makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya Zimbabwe, taarifa ambayo imethibitishwa na mwanadiplomasia wa huo.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Februari, Umoja wa Ulaya uliachia mali na Viza za kusafiria zilizozuiwa dhidi ya Makampuni makubwa ya nchini Zimbabwe na mtu mmoja mmoja baada ya kuridhishwa kuwepo kwa mchakato wa kuridhisha wa kura ya maoni ya mwezi March juu ya Katiba mpya.

Uamuzi wa kuondoa vikwazo hivyo unahitaji baraka zote kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Awali Zimbabwe iliwekewa vikwazo mwaka 2002 kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa, ukiukwaji wa haki za binaadam na kushindwa kusimamia uchaguzi ulio huru na haki.

Katika hatuwa nyingine rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe ameahidi jana Jumanne kuzidisha kasi hatua yake juu ya "uzawa" na  "uwezeshaji" wa kiuchumi  kulazimisha wawekezaji wa kigeni kwa kuuza zao kwa washirika wa ndani kushiriki kikamilifu katika kampuni zenye matawi yake nchini Zimbabwe.

Rais Mugabe ameonya kwamba mpango huo utaongezeka mara dufu. Mugabe mwenye umri wa miaka 89 ambaye alichaguliwa kwa muhula mpya wa miaka mitano, ambaye ametowa kaulihiyo jana wakati akizindua shughuli za bunge.