MALI-SHEREHE

Sherehe za kuapishwa kwa rais wa Mali kufanyika leo ma rais kutoka katika mataifa zaidi ya 15 kuhudhuria

Rais mpya nchini Mali Ibrahim Bubakar Keita
Rais mpya nchini Mali Ibrahim Bubakar Keita Mali actu

Mfalme wa Morroco Muhamed VI na ma rais wengine watano wa bara la Afrika wamewasili jana jijini Bamako ambako wanasubiriwa marais wengine kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, televisheni ya kitaifa ya Mali imeeleza.

Matangazo ya kibiashara

Mfalme Mohamed VI amepata mapokezi ya nguvu wakati aliposhuka kwenye ndege na kupokelewa na rais Keita.

Duru kutoka nchini humo zaarifu kuwa rais Keita amewapokea pia marais: Denis Sassou Nguesso (Congo Brazaville), Moncef Marzouki (Tunisia), Idriss Deby Itno (Tchad), Mahamadou Issoufou (Niger), Alpha Condé (Guinéa Konakry).

Wanasubiriwa pia marais wengine jijini Bamako ambao wanataraji kuwasili leo wakiwemo: François Hollande (Ufaransa), Alassane Ouattara (Côte d'Ivoire), Blaise Compaoré (Burkina Faso), Macky Sall (Sénégal), Mohamed Ould Abdel Aziz (Mauritania), Goodluck Jonathan (Nigeria), Thomas Boni Yayi (Bénin), Ali Bongo Ondimba (Gabon), Jacob Zuma (Afrika Kusini),

Ujumbe kutoka katika mataifa mbalimbali ulimwenguni unasubiriwa jijini Bamako kutoka Uturuki, Qatar, Iran, Urusi, Marekani pamoja pia na wajumbe kutoka katika taasisi za kimataifa.

Sherehe hizo zitafanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa March 26 jijini Bamako wenye uwezo wa kupokea watu elfu 55 ambapo rais Keita athutubia pamoja pia na marais wengine wanne.