Kansela wa Ujerumani Merkel akubali kuunda serikali ya muungano
Chama cha kansela wa ujerumani, Angela Merkel cha Conservative, kinaelezwa kupata ushindi wa kihistoria baada ya miongo miwili licha ya kushindwa kufikisha nusu ya kura ambazo zingekiwezesha chama hicho kuunda Serikali, matokeo ya awali yanaonesha hivyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Chama cha kansela Merkel cha Christian Democratic Union CDU na kile cha Bavarian kinachounda nae serikali kwa pamoja wamepata asilimia 41.5 ya kura huku chama cha Social Democrats SPD kikipata asilimia 25.7
Kansela Merkel amewataka wafuasi wake kusherehekea ushindi huo ambao utamuwezesha kuongoza kwa awamu nyingine.
Iwapo matokeo haya yatathibitishwa rasmi na tume ya uchaguzi basi ni wazi muungano wa chama cha kansela Merkel hawajaweza kuunda Serikali na badala yake watalazimika kutafuta muungano wa vyama vingine kutekeleza lengo lao.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa bado wananchi wa Ujerumani wanaimani na Kansela Merkel na ndio maana wamempigia kura nyingi.