MISRI-CAIRO

Muslim Brotherhood chapigwa marufuku na mali zake kustaafishwa

Mabango yakionesha picha ya raisi Morsi kipindi cha maandamano nchini humo.
Mabango yakionesha picha ya raisi Morsi kipindi cha maandamano nchini humo. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Mahakama nchini Misri imepiga marufuku shughuli zote za chama cha Muslim Brotherhood, na kuagiza kustaafishwa kwa mali zinazomilikiwa na chama hicho .

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unakuja mwezi mmoja baada kufanyika kwa Oparesheni ya kuwasaka wafuasi wa Muslim Brotherhood waliokuwa wamepiga kambi jijini Cairo kutaka kurudishwa madarakani kwa kiongozi wao Mohammed Morsi.

Hata hivyo, chama cha Muslim Brothehood kina uwezo wa kuwasilisha uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa.

Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood walikuwa katika maandamano makubwa katika kipindi cha mwezi uliopita wakipinga kuondolewa madarakani kwa raisi Mohamed Morsi hatua ambayo ilitekelezwa na majeshi ya nchi hiyo.