Viongozi Afrika waitaka DRC kuhakikisha inafanikisha mkataba wa maelewano na kundi la waasi wa M23
Viongozi wa bara la Afrika wameitaka serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23 kufikia mkataba wa maelewanao katika mazungumzo yanayoendelea jijini Kampala ili kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.
Imechapishwa:
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinsasha na waasi wa M 23 yalianza tarehe 10 mwezi uliopita lakini hakuna matunda yeyote ambayo yameonekana.
Umoja wa Mataifa unasema amani Mashariki mwa DRC ni muhimu sana kwa amani ya nchi za Maziwa Makuu.
Mary Robinson Balozi wa Umoja wa Mataifa katika Matifa ya Maziwa Makuu amesema amefurahishwa na tamko la Maraisi wa Afrika wanaotaka mazugumzo ya Kampala yamalizike haraka na mkataba upatikane ili uanze kutekelezwa.
Umoja wa Mataifa umeendelea kusisistiza kuwa mazungumzo ya amani ndio njia pekee ya kumaliza machafuko Mashariki mwa DRC mbali na utumizi wa nguvu za kijeshi kuwapokonya waasi silaha.