SYRIA

Machafuko yashika kasi nchini Syria huku viongozi wa dunia wakiendelea kuvutana kuhusu kuichukulia hatua

Viongozi wa dunia wanaokutana mjini New York Marekani, wanaendelea kuvutana kuhusu azimio la kuchukua hatua dhidi ya utawala wa Syria, wakati huu wachunguzi wa Umoja huo wakiendelea na uchunguzi kubaini ni upande gani ulitimia silaha za kemikali. 

Syria
Syria ewn.co.za
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa wakati viongozi hawa wakiendelea kuvutana, wanatarajia kupata pigo zaidi kwenye harakati zao za kusaka amani ya kudumu nchini humo kufuatia mgawanyiko mkubwa unaoshuhudiwa ndani ya makundi yanayopigana na Serikali.

Kwa upande wake Martin Oloo mchambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa akiwa Juba nchini Sudan Kusini yeye anaona kuwa licha ya uchunguzi huu mpya haoni kama kutakuwa na jambo jipya.

Katika hatua nyingine kumeripotiwa mapigano makali kwenye mji wa Deraa na Allepo pamoja na majimbo mengine kati ya vikosi vya Serikali na wapiganaji wa jeshi huru la Syria ambapo upinzani umeeleza kuwa unalenga kudhibiti mpaka wa nchi hiyo na Jordan.