SYRIA

Rais Assad asisitiza kuwa yuko tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kudhibiti silaha za kemikali nchini Syria

Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad allinstantnews

Rais wa Syria Bashar Al Assad kwa mara nyingine amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kudhibiti silaha zake za kemikali. 

Matangazo ya kibiashara

Rais Assad ametoa hakikisho hilo wakati akihojiwa na runinga moja kutoka nchini Venezuela na kusema kuwa hakuna kikwazo chochote kwa serikali yake kuwasilisha silaha zake kwa Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyokubaliwa kati ya Urusi na Marekani.

Kauli ya Assad unakuja kipindi hiki watalaam wa Umoja wa Mataifa wakirudi nchini humo kuendelea na uchunguzi wao kuhusu matumizi ya silaha za kemikali katika maeneo kumi na manne yanayodhaniwa kuwa silaha hizo zilitumiwa.

Katika hatua nyingine, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataufa linaanda azimio kuhusu Syria baada ya muafaka kati ya Urusi na Marekani kutaka Syria kuwasilisha silaha zake kwa Umoja wa Mataifa ili kuangamizwa.

Marekani imekuwa katika mstari wa mbele kuituhumu serikali ya Assad kutumia silaha za kemiali dhidi ya raia wasiokuwa na hatia tuhuma ambazo serikali ya Damascus imekanusha.

Rais Barrack Obama alisitisha mpango wa jeshi la taifa hilo kuishambulia Syria baada ya kukubaliana na Urusi kuhusu mpango wa kuitaka Syria kukubali silaha zake kuchungumzwa na kuharibiwa na Jumuiya ya Kimataifa.