SYRIA-MAREKANI-URUSI

Wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN, kupiga kura hii leo kuhusu azimio la kuteketeza silaha za kemikali nchini Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kupitia wanachama wake watano wa kudumu wanatarajiwa kupiga kura kupitisha azimio la pamoja la Marekani na Urusi la kutaka kuangamizwa kwa silaha za kemikali zinazomilikiwa na serikali ya Syria. 

Katibu mkuu wa UN  Ban Ki-moon,akiwa na wajumbe wengine wa umoja huo.
Katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon,akiwa na wajumbe wengine wa umoja huo. huffingtonpost.com
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa hayo matano wanatarajiwa kupiga kura hiyo inayokuja baada ya Marekani na Urusi kufikia muafaka juu ya suala la kuteketeza silaha hizo zinazodaiwa kutumika katika shambulio mjini Damascus na kuua raia wasio na hatia.

Marekani ambayo hapo awali ilishakuwa tayari kutumia nguvu ya jeshi kuushambulia utawala wa rais Bashar Al Assad inaonekana kufurahishwa na azimio hilo ambalo linalenga kukomesha matumizi ya silaha za kemikali nchini humo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Baraza la Taifa la Upinzani nchini Syria Khaled Saleh anayehudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa UN akiwakilisha waasi amesema kuwa anatumai kuwa azimio hilo linafikiwa.

Mataifa ya Magharibi yameendelea kufanya ushawishi wa hali ya juu katika kuhakikishwa wanapata uungwaji mkono kwenye mchakato wao wa kutaka kuteketeza silaha za kemikali zinazomilikiwa na Syria wakidai zimekuwa zikiua wananchi wasio na hatia.