IRAQ

Watu wapatao 47 wamepoteza maisha nchini Iraq kwenye wimbi la mashambulizi ya kujitoa mhanga

Mabaki ya gari yaliyotumika kwenye shambulizi la kujitoa mhanga Jijini Baghdad nchini Iraq
Mabaki ya gari yaliyotumika kwenye shambulizi la kujitoa mhanga Jijini Baghdad nchini Iraq

Watu wapatao arobaini na saba wamepoteza maisha kwenye wimbo jipya la mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotekeleza leo nchini Iraq na kuwaacha watu zaidi ya mia moja hamsini na sita wakijeruhiwa wengi wao vibaya.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ya kujitoa mhanga yametekelexzwa kwa kutumia mabomu tisa yaliyokuwa yametekewa kwenye magari tisa tofauti na kulenga zaidi Jiji la Baghdad katika maeneo yanayokaliwa zaidi ya Waumini wa Kishia.

Taarifa kutoka Jijini Baghdad zinaweka bayana mashambulizi hayo ya mabomu yamepiga sehemu nane tofauti na kuleta madhara kwenye soko la mbogamboga na kusababisha vifo vya polisi saba wakiwemo wanajeshi wawili na wengine kumi na sita wakijeruhiwa.

Maeneo yaliyoathirika zaidi na mashambulizi hayo mabaya zaidi kutekelezwa katika siku za hivi karibuni ni viunga vilivyopo kwenye Jiji la Baghdad ikiwemo Habibiya, Sabaa Al Bour na Kazimiyah.

Sehemu hizo zilizoshambuliwa huwa zinakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu na ngome imara ya waumini wa Kishia ambao wamekuwa walengwa wakubwa wa mashambulizi yanayofanywa na makundi ya Kisunni.

Vyombo vya usalama nchini Iraq vimethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo baya na juhudi za kuwaska waliohusika vimeazishwa huku usalama ukiendelea kuimarishwa katika Jiji lote la Baghdad.

Hadi kufika sasa hakuna Kundi lolote lililotangaza kuhusika kupanga na hatimaye kutekeleza shambulizi hilo lililoongeza hali ya wasiwasi juu ya usalama wa wananchi wa Taifa la Iraq.

Shambulizi lenyewe limekuwa likitajwa kama la kulipiza kisasi kutokana na Ijumaa kutekelezwa kwa mashambulizi mawili ya mabomu jirani kabisa na Msikiti Mkubwa wa Sunni uliopo kwenye Jiji la Baghdad na kuchangia vifo vya waumini sita.

Matukio haya yanafanya idadai ya watu waliopoteza maisha kwenye mashambulizi yaliyofanyika nchini Iraq mwezi Septemba kuzidi kuchupa kwani takwimu zinaonesha mwezi Agosti watu zaidi ya mia nane walipoteza maisha.