KENYA-ICC-AU

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latupilia mbali pendekezo la AU kutaka kesi za viongozi wa Kenya ziahirishwe

Raiswa Kenya  Uhuru Kenyata na naibu wake William Ruto
Raiswa Kenya Uhuru Kenyata na naibu wake William Ruto AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC jana Ijumaa limetupilia mbali ombi la Umoja wa Afrika la kutaka kesi za uhalifu dhidi ya binadamu zinazowakabili viongozi wakuu wa Kenya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ziahirishwe. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imezua mtafaruku ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika yamegadhabishwa na hatua hiyo huku wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakichukizwa na tuhuma za Kenya na washirika wake kuwa wamelidhalilisha bara hilo.

Azimio la Afrika lilitoa wito kwa baraza hilo kutumia mamlaka yake maalum kuahirisha kesi ya Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto kwa mwaka mmoja.

Viongozi hao wawili wanatuhumiwa kwa kuchochea machafuko ya kisiasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1,100 walipoteza maisha.

Hata hivyo azimio hilo lilipata kura saba pekee pungufu ya kura mbili ambazo zingetimiza idadi ya kura tisa zilizotakiwa ili kupitisha azimio hilo kati ya wanachama 15 wa baraza hilo.

Mataifa nane wajumbe wa baraza , wote wakiwa wanachama wa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC ama waungaji mkono wa mahakama hiyo ikiwa ni pamoja na Uingereza ,Ufaransa na Marekani, hawakupiga kura na kusababisha kushindwa kwa jitihada hizo.