KENYA

Serikali ya Kenya yawatuhumu wapinzani kueneza propaganda dhidi ya kesi inayowakabili viongozi wake katika mahakama ya ICC

Reuters/Noor Khamis

Joto la kisiasa linazidi kupanda kuhusu kesi za uhalifu dhidi ya binadamu zinazomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika mahakama ya ICC ya mjini Hague Uholanzi, ambapo sasa serikali ya Kenya inatuhumu muungano wa upinzani kwa kueneza propaganga kuhusu kesi hizo, jambo ambalo muungano huo umepinga vikali. Taarifa ya Mwanahabari wetu wa Nairobi, Paulo Silva inafafanua zaidi.