PAKISTAN-TALIBAN-MAREKANI

Marekani yashambulia Pakistan,3 wauawa akiwemo kiongozi wa mtandao wa Haqqani

Kiongozi wa kiroho wa kundi la Haqqani Maulana Ahmad Jan,ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi hilo,lililolenga eneo la Haqqan
Kiongozi wa kiroho wa kundi la Haqqani Maulana Ahmad Jan,ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi hilo,lililolenga eneo la Haqqan flickr.com

Shambulizi lililotekelezwa na majeshi ya Marekani kaskazini magharibi mwa Pakistan limesababisha vifo vya watu watatu akiwemo kiongozi mkubwa wa mtandao wa kigaidi wa Haqqani maafisa wamethibitisha ikiwa ni shambulizi la pili kulenga eneo lenye matukio ya uvunjifu wa sheria.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la Kombora lililenga shule ya kidini ambayo wapiganaji na maafisa usalama wamesema ni eneo la Magaidi huku wakilaumu mashambulizi mengine jirani na Afghanstan katika wilaya ya Hangu jimboni Khyber Pakhtunkhwa.

Chanzo kimoja cha mtandao wa kigaidi wa Haqqani ameiambia AFP kwamba kiongozi wa kiroho wa kundi la Haqqani Maulana Ahmad Jan, alikuwa miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi hilo,lililolenga eneo la Haqqan la kupumzikia wapiganaji waliokuwa wakipambana na majeshi ya NATO huko Afghanistan.

Mapema mwezi huu mkuu wa masuala ya kifedha katika mtandao huo Nasirudddin Haqqani, aliuawa katika mazingira yenye utata katika kijiji kimoja huko Islamabad.

Kama ilivyo ada kwao baada ya shambulizi hilo serikali ililaani kwa kuona ni ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchini humo na kikwazo cha jitihada za kukomesha makundi ya wapiganaji yanayomiliki silaha.

Shambulizi la Alhamis linakuwa la kwanza kulenga jimboni Khyber Pakhtunkhwa huku awali likilenga nje ya Banu.

Shambulizi hilo ni la kwanza nchini Pakistan tangu Kiongozi wa kundi la Taleban la Pakistan Hakimullah Mehsud alipouawa katika shambulizi kama hilo huko kaskazini mwa Waziristan mapema mwezi huu.